
Katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora, tumefungua Kampasi (Ndaki) mpya eneo la Kiluvya Madukani. Ndaki hii itaendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu ya Uandishi wa Habari.
Sanjari na programu ndefu za Astashahada na Stashahada ya Uandishi wa Habari, vilevile kozi fupi zitaendelea kufundishwa kwenye ndaki hii.
Hivyo tunaendelea kuwakaribisha kwa Mafunzo halisi na bora ya vitendo.